Ilifanyika katika ya Mhashamu Baba Askofu Eusebius Nzigirwa msaidizi wa jimbo kuu la Dar es salaam tarehe 06/10/2013 ,
Ni harambee ya kanisa hili la Katoliki lililopo Kibiti linaloendelea kujengwa.
Baada ya kufika mgeni rasmi Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Baba Askofu alifungua shughuli kwa sala takatifu ya kubariki shughuli nzima mwanzo mpaka mwisho
Kisha Father Lupindu alitoa taarifa ya kanisa linavyoendelea kujengwa mpaka lilipofikia sasa na kiasi gani kinatakiwa ili kumalizia finishing.
Mgeni Rasmi Waziri Mkuu aliongea na kutoa mwongozo wa Harambee hiyo.
Kisha Waziri Mkuu alimwita Mc Peter Mwampondele na Father Lupindu kuwa wagawe fomu kwa wote walioudhulia tayari kwa kuchangia chochote walichonacho.
Na fomu ziliendelea kujazwa
Alikuwepo pia Mheshimiwa Waziri Mary Nagu (MB) na Mheshimiwa Reginald Mengi
Meza kuu nao walijaza fomu hizo
Mc Peter akipewa mwongozi na Baba Askofu
Meza ya mahesabu waliendelea kuweka kumbukumbu vizuri kwa fomu zilizojazwa
Mc Peter akipewa sifa na Waziri Mary Nagu kwa kazi nzuri anayofanya
Mc Peter na Father Lupindu wakipewa mwongozo na waziri mkuu.
Mc Peter wakijadiliana na Mheshimiwa Reginald Mengi.
Mc Peter wakijadiliana na Mheshimiwa Reginald Mengi.
Mc Peter wakijadiliana na Mheshimiwa Reginald Mengi.
Kisha Mke wa Waziri Mkuu Mama Pinda alimwita Father Lupindu kumpa zawadi ya kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya.
Ambapo alikabidhiwa box la Rozari
Waziri mkuu akitoa taarifa ya harambee hiyo ambapo ilihitajika milioni mia mbili ili kumaliza ujenzi wa kanisa kubwa la Kibiti na ilipatika yote kwenye harambee hiyo...
Kisha Father Lupindu nae aliwapa zawadi meza kuu ya vikombe ambavyo hubadilika rangi pindi ukiweka maji ya moto
Hapa walijaribu kuweka maji kwenye kikombe cha waziri mkuu
Hapa kikibadilika rangi
Hapa father lupindu akiwaonyesha waheshimiwa
Waziri mkuu alimwita Reginald mengi nae kumpa zawadi ya kikombe kwa kufika kwake kwenye harambee hiyo..
Pia alimpa zawadi ya kikombe mheshimiwa waziri Mary Nagu
Waziri Mkuu alimfuata katibu Mkuu kiongozi mstaafu wa ofisi ya rais Mzee Rupia kumpa zawadi ya kikombe pia.
Kisha waziri mkuu alikata keki iliyojengwa kwa muundo wa kanisa baada ya malengo ya haraambee kukamilika.
Hapa Mhashamu Baba Askofu Nzigirwa akitoa sala ya kwenda meza kuu ya chakula.
Hapa shughuli ilifika tamati na waheshimiwa walianza kutoka
Mzee Reginald Mengi nae alimpongeza Mc Peter kwa kazi nzuri sana.
Na hapa Mc akiagwa na Mheshimiwa waziri Mary Nagu
Waziri mkuu na Mkewe mama Pinda wakitoa neno kwa waumini waliohudhuria harambee hiyo.
Waziri mkuu akiwaaga Masister wa meza ya mahesabu
Waziri mkuu alimwambia Mc Peter Bravo kwa kuendesha harambee hiyo vizuri sana.
safi sana ...hongera kijana kwa kazi nzuri
ReplyDeletehahahahahaha thanks comrade, unajua shughuli nzito kama hizo inabidi kutunza heshima kwa umakini wa hali ya juu.
Delete