Wednesday 11 September 2013

Uzinduzi wa wimbo "anzen unten" Endesha kwa uangalifu, Serena Hotel Dar, 09/09/2013

 Siku ya uzinduzi wa wimbo endesha kwa uangalifu "anzen unten" uliofanyika Serena Hotel Dar es salaam, THT Band pamoja na DJ Amadi kutoka Stevangie Entertainment ndio waliosimamia show nzima.

 
 Mzee wa jahazi kibonde ndie aliyekuwa MC wa shughuli nzima
 
 Balozi wa japan nzini Tanzania alikuwepo na ndiye mgeni rasmi. hapa akitoa ufafanuzi maana ya anzen unten.
 
 Mdau mkuu wa usalama barabarani walikuwepo katika uzinduzi huo


 Ni vijana watatu ndio walioimba wimbo huo, hapa waliitwa mbele na MC kibonde kutambulishwa ambao ni Barnaba, Recho katikati na Tony
 
 Hapa wakiimba huwo wimbo endesha kwa uangalifu anzen unten
 
 

 Recho mwanadada mwenye sauti nzuri
 
 Hakika wimbo ni mzuri sana

 Pia ilionyeshwa live kwenye screen kubwa ya projector

 Hapa mc waliwaita wadau filamu ambao ndio walioitengeneza video hiyo, ambapo wa kwanza kushoto ni mweshimiwa Mtitu na wadau wa filamu kutoka japan
 
 Barnaba Boy "smart boy"
 
 Mtitu akifafanua walivyoitengeneza video ya anzen unten
 
 Joshua mpiga bazzi gitaa aliongoza timu mzima ya THT walioshilikiana na DJ Amadi kutoka Stevangie Entertainment katika burudani nzima. 
 
 Sound system ilifungwa na Stevangie Entertainment chini ya DJ Amadi
 
 Wadau mbalimbali wa filamu nchini walikuwepo
 
DJ Amadi kutoka stevangie entertainment

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...